Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yawapongeza kundi la waasi Darfur kwa uamuzi wao kukomesha matumizi ya watoto katika jeshi

UNAMID yawapongeza kundi la waasi Darfur kwa uamuzi wao kukomesha matumizi ya watoto katika jeshi

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kuhusu Darfur, UNAMID, umepongeza uamuzi wa mojawepo wa makundi makubwa zaidi ya waasi katika jimbo hilo la Sudan kukomesha kuajiri na kutumia watoto kama wanajeshi.

Kufuatia mazungumzo na viongozi wa ujumbe wa UNAMID, kundi la waasi la Justice and Equality Movement, (JEM), limekubali kuweka mbinu ya kuwatambua watoto ambao wanahusika na vikosi vyake, ili kuwaondoa jeshini na kuwarejesha katika maisha ya uraia.

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na UNAMID, kundi hilo limetoa amri ya kuwataka wafuasi wake wote kuheshimu kikamilifu sheria za kimataifa na za kitaifa zinazohusiana na ulinzi wa watoto katika vita vya silaha. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)