Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makundi ya kigeni vitani nchini Syria

Makundi ya kigeni vitani nchini Syria

Makundi wa wapiganaji ya kigeni ni kati ya yale yanayoipiga vita srikali ya Syria kwa mujibu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayochunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo. Tume hiyo inasema kuwa makundi hayo yamejiunga na yale yanayoipinga serikali ikiongeza kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kutoka pande zote umeongezeka huku makundi yanayoipinga serikali yakiendelea kuongezeka.

Akihutubia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva mkuu wa tume hiyo Paulo Pinheiro amesema kuwa mashambulizi dhidi ya raia ni jambo la kila siku kwenye miji ya Aleppo, Damascus, Dera, Latakia, Idlib na Homs.

(SAUTI YA PAULO PINHEIRO)