Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi maalum kuhusu Syria, Lakhdar Brahimi azuru Damascus

Mwakilishi maalum kuhusu Syria, Lakhdar Brahimi azuru Damascus

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu ambaye amemrithi Koffi Annan, Lakhdar Brahimi, ameanza ziara yake ya kwanza nchini Syria. Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa amekutana na waangalizi wa zamani wa Umoja wa Mataifa, UNMISS, na timu ndogo ya wafanyakazi ambao watabaki mjini Damascus kusaidia katika huduma za ofisi ya Bwana Brahimi, wakiongozwa na Mokhtar Lamani.

Bwana Brahimi amekutana baadaye na Mabalozi wa Urusi na Uchina, pamoja na wawakilishi Muungano wa Mataifa ya Kiislamu, na Shirika la Msalaba Mwekundu. Mnamo siku ya Alhamis, alikutana na Balozi wa Iran Baadaye Ijumaa amekutana na wawakilishi wa kamati ya uratibu wa kitaifa, na Mkuu wa ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadam, OCHA.

Mnamo siku ya Jumamosi, Bwana Brahimi anatarajiwa kukutana na rais Assad, makundi ya upinzani, mabalozi wan chi za Kiarabu, wawakilishi wa mashirika ya umma, Muungano wa Ulaya, na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Adam Abdelmoula.