Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Yemen

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Yemen

Baraza la Usalama limelaani vikali mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa ambayo yamesabisha watu kadhaa kupoteza maisha akiwemo waziri wa ulinzi

Gari lilikuwa limeengeshwa kando kando ya msafara wa Waziri wa ulinzi lililipuka na kusababisha uharibifu mkubwa. Duru za vyombo vya habari zinasema kuwa msafara wa Waziri Nasir Ahmad aliyekuwa akipita karibu na majengo ya serikali.

Katika taarifa yake, baraza la usalama limeyaita mashambulizi hayo kama tukio la kuugofyesha na kulaani kwa nguvu zote.

Baraza hilo limetuma salama za rambirambi kwa ndugu na jamaa waliofikwa na tukio hilo pamoja na serikali ya Yemen.