Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada zaendeshwa Tanzania kukabiliana na matatizo ya watoto wa mitaani

Jitihada zaendeshwa Tanzania kukabiliana na matatizo ya watoto wa mitaani

Pamoja na juhudi kubwa zinazochukuliwa na mashirika ya kiraia kukabiliana na ongezeko la watoto wa mitaani, nchini Tanzania hata hivyo juhudi hizo bado zinaendelea kugonga mwamba na wakati huu kunashuhudia ongezeko kubwa la watoto hao wakiranda randa mitaani. Kuna mambo mengi yanayowasukuma watoto hao kutumbukia kwenye hali hiyo,,, lakini suala la umaskini kwenye familia nyingi ndilo linalichukua nafasi ya juu

Hata hivyo habari njema ni kwamba sehemu ya kundi hilo la watoto hao hivi sasa linaendesha harakati mpya kupitia vipaji vyao vya uimbaji mziki. Kwenye makala yetu hii leo George Njogopa anatupia jicho jitihada zilizochukuliwa na baadhi ya watoto hao waliamua kuingia studio na kufyatua kibao chao.