Wanaharakati wa haki za binadamu wanateswa bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi ya wanaofanya hivyo: Ban

13 Septemba 2012

Makumi ya watu katika angalau nchi 12 kote duniani wamekabiliwa na mateso makubwa ya kulipiza kisasi na vitisho katika kipindi cha mwaka mmoja ulopita, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon.

Ripoti hiyo inasema, wanaharakati hao wa haki za binadamu waliteswa, walifungwa bila kufikishwa mahakamani, au kupigwa, huku wengine wakipigwa marufuku kusafiri, kuitwa wasaliti na kukabiliwa na vitendo tofauti vya kikatili, hasa mikononi mwa vyombo vya usalama vya kitaifa.

Bwana Ban amesema, ni jambo la kuvunja moyo, kwamba serikali husika hazikutaka kufanya uchunguzi na kuwafikisha waliotekeleza vitendo hivi mbele ya sheria. Katika taarifa yake kwa jopo la Baraza la Haki za Binadamu linalohusika na mateso ya aina hii, Bwana Ban ametoa wito kwa serikali kote duniani kufanya juhudi zaidi kuwalinda watu ambao hushirikiana na Umoja wa Mataifa katika uwanja wa haki za binadam.

(SAUTI YA BAN)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter