Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watafakari kutuma vikosi huru DRC

UM watafakari kutuma vikosi huru DRC

Umoja wa Mataifa umesema kuwa bado unaendelea kutafakari juu ya uwezekano wa kutuma vikosi vya askari wasiofungamana na upande wowote katika eneo linalokabiliwa na mzozo mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous,ambaye kwa sasa yupo katika ziara ya kutembelea eneo la maziwa makuu.

Kunauwezekano mkubwa Baraza la Usalama likapitisha mpango wa kutumw akwa vikosi huru kwenye eneo hilo ili kuzima uasi unaendelea kusumbua eneo hilo.Hata hivyo kabla ya kufikia hatua hiyo kuna ulazima wa kutajwa vipaumbele vitakavyozingatiwa iwapo jeshi hilo litatumwa nchini humo.

Bwana Ladsous yuko katika ziara ya eneo la maziwa makuu akikutana na maafisa wa serikali pamona na maafisa wa ofisi za kimataifa . Pia ametumia fursa hiyo kutathmini hali ya mkwamo inayoliandama eneo hilo.