Shambulio dhidi ya hoteli ya Jazeera Mogadishu lalaaniwa vikali na UM

13 Septemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio dhidi ya hoteli ya Jazeera mjini Moghadishu ambako Rais mpya wa Somalia aliyechaguliwa Hassan Sheikh Mohamud alikuwa akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Kenya profesa Samuel Ongeri mbele ya vyombvo vya habari vya kimataifa siku ya Jumatano.

Katika taarifa yake Ban amesema anashawishika kwamba mashambulizi kama hayo hayatobadili mafanikio yaliyopatikana karibuni au kudhoofisha nia ya Wasomali ya kupata amani na usalama nchini mwao. Amerejea kusema Umoja wa mataifa utaendelea kumunga mkono na kumsaidia Rais Mohamud na wato wote wa Somalia katika juhudi zao za kuleta amani. Balozi Augustine Mahioga ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter