Ban na UM kwa ujumla walaani shambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani Libya

13 Septemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani Benghazi nchini Libya ambayo yamesababisha kifo cha wanadiplomasia wanne akiwemo balozi wa Marekani nchini humo, pamoja na wafanyakazi wa ubalozi ambao ni raia wa Libya.

Ban amesema amestishwa saana na shambulio hilo na ametuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Marekani , familia za waliopoteza maisha na serikali ya Libya. Katika taarifa yake baraza la usalama limesema linangana na Katibu Mkuu kulaani tukio hilo na kuwafariji familia za walioathirika. Naye Rais wa mkutano wa upokonyaji silaha unaoendelea mjini Geneva Balozi Hellmut Hoffman akilaani shambulio hilo amesema vifo vya wanadiplomasia hao ni kumbusho kwamba mchakato wa haraka wa kurejesha amani na tulivu Mashariki ya Kati unahitajika.

(SAUTI YA HELLMUT HOFFMAN)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter