Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Tarek Mitri kama mjumbe wake maalumu nchini Libya

Ban amteua Tarek Mitri kama mjumbe wake maalumu nchini Libya

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Tarek Mitri kutoka Lebanon kama mjumbe wake mpya na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL. Bwana Mitri anachukua mahala pa Ian Martin ambaye anakamilisha majukumu yake tarehe 14 mwezi Oktoba mwaka huu.

Kupitia kwa msemaji wake Ban amempongeza bwana Martin kwa kazi ambayo ameitekeleza kwa muda wote ambao mahudumu. Mitri ni msomi na amehudumu kwenye wizara kadha katika serikali ya Lebanon kati ya mwaka 2005 na 2011. Mitri pia amefanya kazi kwenye shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO mjini Beirut pamoja na kwenye baraza la kimataifa la makanisa mjini Geneva na mashariki ya kati.