Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa shughuli za kulinda amani wa UM azuru nchi za maziwa makuu

Mkuu wa shughuli za kulinda amani wa UM azuru nchi za maziwa makuu

Mkuu wa shughuli za kulinda amani  katika Umoja wa Mataifa, anafanya ziara katika nchi za Maziwa Makuu  kujaribu kutafuta suluhu  la mapigano mashariki mwa Congo.

Akiwa mjini Kigali Rwanda jumatano, Bwana Herve Ladsous amezitaka pande husika kuhakikisha mapigano yanamalizika mashariki mwa Congo, na hasa kujizuwia kuunga mkono makundi ya waasi.

Amechukuwa fursa ya ziara yake hiyo kuwaalika viongozi wa nchi hizo kushiriki katika mkutano wa viongozi wa nchi za ukanda huo, wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadae mwezi huu mjini New York.

Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga anaripoti.