Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani inapaswa kuwajali watu wa asili:UM

Marekani inapaswa kuwajali watu wa asili:UM

Marekani inapaswa kuanzisha mbinu mpya ili kukaribisha majadiliano ya sura ya maridhiano dhidi ya kundi la watu wa wazawa ambao kwa sasa wanakabiliwa na hali ya mkwamo.

Katika taarifa yake, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wazawa, amesema kuwa kundi hilo limetoa mchango mkubwa kwa uhai wa taifa hilo na amesema kwamba sasa ni wakati muafaka matatizo ya kihistoria yanayowaandama watu hao yanapatiwa ufumbuzi.

Bwana James Anaya amekumbusha historia ya watu hao ikiwemo wale wazawa wa Alaska pamoja na wahindi asilia yaani red indiani namna walivyofanikisha ustawi wa taifa hilo lakini wameendelea kuachwa nyuma.

Amesema kuna haja ya kuanza kuwamulika watu wa jinsi hiyo ambao historia imeendelea kuwabagua na kuwekwa kando na vipaumbele vya serikali.