Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani vikali mauaji ya Balozi wa Marekani nchini Libya

Baraza la Usalama lalaani vikali mauaji ya Balozi wa Marekani nchini Libya

Mauaji ya Balozi wa Marekani nchini Libya na wafanyakazi wengine watatu yamelaaniwa vikali na Baraza la Usalama.

Balozi J. Christopher Stevens na wafanyakazi wale wengine wamepotiwa kuuawa katika shambulio lililotekelezwa na wanaume watatu wenye silahaha wasiojulikana.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, wanaume hao waliingia katika majengo ya Ubalozi wa Marekani Benghazi kwa sababu wamekasirishwa na video moja iliozalishwa Marekani ambayo inasemekana kumtusi Mtume Mohammed.

Balozi Peter Witting ni Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa September.

(SAUTI YA PETER WITTING)