Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua za Lebanon za kumaliza ghasia

UM wakaribisha hatua za Lebanon za kumaliza ghasia

Maafisa kutoka Umoja wa Mataifa wamekaribisha hatua za kiusalama zilizochukuliwa nchini Lebanon ambapo wametaka kuwepo kwa utulivu wa kisiasa. Mzozo unaondelea nchini Syria umechochea ghasia kwenye taifa taifa jirani la Lebanon na kuzua wasi wasi wa taifa hilo kurejea tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 1990. Mwezi uliopita kulishuhudiwa mapigano kati ya waungaji mkono na wanaopinga serikali ya Syria kwenye mji mkuu wa Lebanon Beirut ambapo watu 12 waliuawa na wengine kutekwa nyara.

Hata hivyo mratibu wa masuala ya Umoja wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Derek Plumbly alipongeza ripoti zilizosema kuwa baadhi ya waliotekewa nyara wamechiliwa ishara kwam,ba hali inarudi kuwa tulivu.