Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Venezuela kutojiondoa kwenye mkataba wa kulinda haki za binadamu wa mataifa ya Amerika

Pillay aitaka Venezuela kutojiondoa kwenye mkataba wa kulinda haki za binadamu wa mataifa ya Amerika

Afisa mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelishauri taifa la Venezuela kutojiondoa kwenye mkataba wa haki za binadamu wa mataifa ya Amerika akionya kuwa hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kwa haki za binadamu kwenye eneo hilo. Kulingana na taarifa kutoka kwa muungano wa mataifa ya Amerika OAS mapema juma hili serikali ya Venezuela iliufahamisha muungano huo juu ya uamuzi wake kupitia kwa njia ya barua na pia kuutupilia mbali muungano huo. Mkataba huo ulionza kutumika mwaka 1978 unaangazia haki za binadamu ambazo mataifa hayo yamekubaliana kuheshimu.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Ofisi ya mkuu wa haki za binadamu ni kwamba Venezuela imechukua uamuzi huo baada ya azimio zilizopitishwa na baraza la haki za binadamu mjini Genevaya za kuhakikisha kuwepo ushirikino na mashirika ya haki za binadamu ya kimaeneo na ya kimataifa.