Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia bado inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya vita:UM

Liberia bado inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya vita:UM

Taifa la Liberia limepiga hatua kubwa katika kujenga taasisi zake, katika kuufufua uchumi na kwenye demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenye lakini hata hivyo linahitaji kuangazia zaidi kwenye changamoto ambazo bado zimesalia zikiwemo sheria, mabadiliko kwenye sekta ya ulinzi na uwiano. Hii ni kwa mujibu wa mjumbe maalum na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL Karin Landgren.

Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Landgren amesema kuwa tangu mwaka 2003 Liberia taifa la Liberia limefanya mabadiliko makubwa yakiwemo ya kidemokrasia na ya kuhakikisha kuwepo kwa amani. Amesema kuwa uchaguzi wa ubunge na urais wa mwaka 2011 ulionyesha uwezo wa taifa hilo wa kutekeleza masuala yake ya kisiasa.