Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushahidi dhahiri umepatikana kuhusu utesaji nchini Misri:UM

Ushahidi dhahiri umepatikana kuhusu utesaji nchini Misri:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji, ukatili, unyama na udhalilishaji bwana Juan E. Mendez ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa matumizi ya kile serikali inachokiita mahakama za usalama Misri. Mwakilishi huyo anasema mahakama hizo zimewahukumu wanaume watatu kifo kutokana na makosa ya ugaidi kwa madai kwamba walikiri, kukiri kunakodaiwa kufanyika kutokana na kuteswa.

 Bwana Mendezi amesema serikali ya Misri ina wajibu wa kuhakikisha kwamba maelezo yoyote ynayotolewa kutokana nan kuteswa hayatumiki kama ushahidi katika kesi yoyote na katika mazingira yoyote ikiwemo katika mazingira ya mahakama za kijeshi. George Njogopa na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)