UNICEF na EU wanatoa kipaumbele kwa watoto wakati wa dharura:

11 Septemba 2012

Umoja wa Ulaya utaendelea kutoa kipambele cha ufadhili wake kwa watoto kwenye masuala ya dharura licha ya changamoto za kichumi zilizopo amesema kamishina wa ushirikiano wa kimataifa , misaada ya kibinadamu na kukabili majanga wa Umoja huo Kristalina Georgieva.

Bi Georgieva ameyasema hay oleo akiihakikishia bodi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakati wa hotuba yake ambayo ni ya kwanza kwa kamishina wa Umoja wa Ulaya kuitoa kwa bodi ya wakurugenzi ya UNICEF.

Tume ya Umoja wa Ulaya ni mshirika mkubwa wa UNICEF na wanafanya kazi pamoja katika nchi 27 zilizoathirika na masuala ya dharura au zilizotoka vitani. Ushirika baina ya UNICEF na tume hiyo ya Ulaya ECHO ulianza 1992 na mwaka jana ECHO ilitoa zaidi ya Euro milioni 70 kwa UNICEF ili kusaidia masuuala ya kibinadamu duniani kote.

Kamishina huyo ya Umoja wa Ulaya amesisitiza kwamba raia wa muungano wa Ulaya wanaunga mkono mipango ya ufadhili ya kuwasaidia wanaohitaji msaada zaidi hasa watoto, wakitolea mfano kura ya karibuni inayodhihirisha kwamba watu tisa kati ya 10 wanaamini misaada ya kibinadamu ni muhimu saana.

Kimataifa UNICEF ni mshirika mkubwa wa ECHO katika mipango inayohusiana na lishe, na msaada huo umeokoa maisha ya watoto wengo wanaokabiliwa na utapia mlo katika Pembe ya Afrika na Sahel.