Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia lazima ishirikiane kuzikabili changamoto za kimaendeleo:UM

Dunia lazima ishirikiane kuzikabili changamoto za kimaendeleo:UM

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ametaka kuwepo kwa mshikamo wa pamoja ili kuzikabili changamoto zinazoikabili dunia ikiwemo kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi na mikwamo ya kiuchumi.

Akizungumza kwenye kongamano la kimataifa linalofanyika kwa ajili kujadilia namna kufikia kwa pamoja na malengo ya kimaendeleo, Naibu huyo amepuuza mipango ya muda mfupi wakati kunapojitokeza majanga ya muda mrefu.

Amesema dunia haipaswi kuzishughulikia changamoto za muda mrefu kwa kuanzisha mikakati ya muda mfupi.

Ametaka kuongezwa kwa juhudi ili hatimaye kufikia utimilifu wa malengo ya maendeleo ya mellenia ambayo yanamulika kuanzia maeneo ya usalama wa chakula, usawa na kukabili changamoto za kimazingira.