Haki ya mabadiliko ni muhimu kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu:Greiff

11 Septemba 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki ya mabadiliko Pablo de Greiff amezishauri serikali kote duniani kukoma kuchukulia haki ya mabadiliko kama hali iliyo dhaifu.

Akitoa ripoti yake ya kwanza kabisa kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Mjumbe huyo amesema kuwa haki ya mabadiliko sio haki iliyotoweka lakini ni mkakati wa kupata haki na kumaliza ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa mabadiliko.

Amesema ukiukaji wa haki za binadamu hauwezi kumalizwa bila ya kuwepo ukweli na haki. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter