Idadi ya watu walio hatarini nchini Somalia imepungua kwa asilimia 16:OCHA

11 Septemba 2012

Idadi ya watu wanaopitia hali ngumu nchini Somalia imepungua kwa asilimia 16 kutoka watu milioni 2.51 hadi watu 2.12. Hi ni kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA.

Kulingana na OCHA mabadiliko hayo yanatokana ana kujitolea kwa mashirika ya kibinadamu kwa muda wa mwaka mmoja uliopita , mavuno ya mwezi Januari, kuwepo upatikanaji wa maziwa na bei ya juu ya mifugo kwenye sehemu nyingi zenye wafugaji nchini Somalia.

Hata hivyo kwa ujumla hali ya kibinadamu nchini Somalia inasalia kuwa mbaya na hivyo inahitaji kusalia kama ajenda kuu duniani ili kuzuia kupoteza mafanikio ambayo tayari yamepatikana.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter