Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha kuchaguliwa kwa rais mpya Somalia

UM wakaribisha kuchaguliwa kwa rais mpya Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametuma salamu za hongera kwa Bwana Hassan Sheikh Mohamud kufuatia kuchaguliwa kwake kama rais wa taifa la Somalia, katika kura ilopigwa na bunge la taifa hilo mnamo siku ya Jumatatu.

Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema kuteuliwa kwa rais mpya kunahitimisha miaka minane ya kipindi cha mpito kisiasa. Ametoa wito kwa rais huyo mpya kufanya haraka na kuunda serikali inayowakilisha watu wote, yenye kuwajibika, na ambayo inaweza kuanza kazi ya kujenga amani nchini humo.

Naye Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustine Mahiga, amesema kuchaguliwa kwa rais mpya ni hatua kubwa kwenye barabara ya kufikia amani na ufanisi, na kuongeza kuwa hatua hiyo inatoa ujumbe wenye uzito mkubwa kwa bara zima la Afrika na ulimwengu mzima.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)