Uharibifu mkubwa wa hospitali na vituo vya afya washuhudiwa nchini Syria:WHO

11 Septemba 2012

Hospitali na vituo vya afya ni kati ya maeneo muhimu yaliyoharibiwa kwenye mzozo unaondelea nchini Syria kulingana na sirika la afya duniani WHO. Kwenye wilaya ya Homs asilimia kubwa ya hospitali 44 za umma na zile za kibinafsi imeharibiwa na kuacha hopitali 14 tu zikiwa ndizo zinatoa huduma. WHO inasema kuwa hospitali ya kitaifa yenye vitanda 350 mjini Homs imeharibiwa kabisa. Hospitali zilizosalia kwa sasa hazima uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa na pia zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawa. Tarik Jasarevic kutoka WHO anasema kuwa athari za kiafya kwa waliohama makwao zinaongezeka kila siku.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter