Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ateua maafisa wawili kwa ajili ya Mashariki ya Kati na DRC

Ban ateua maafisa wawili kwa ajili ya Mashariki ya Kati na DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza uteuzi wa maafisa kadhaa ambao watajishughulisha na masuala ya uratibu wa amani katika eneo la Mashariki ya Kati na katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC.

Ban amemteua mwanadiplomasia James W.Rawley kuwa mratibu wa zoezi la usakaji wa amani ya kudumu Mashariki ya Kati na wakati huo huo ametangaza kumteua Moustapha Soumaré kutona nchini Mali kuwa mratibu wa vikosi vya kulinda amani DRC.

Bwana Rawley anachukua nafasi iliyoachwa na Maxwell Gaylard ambaye amemaliza muda wake. Na Bwana Soumaré anachukua nafasi ya Fidèle Sarassoro kutoka Ivory Coast ambaye anatazamiwa kumaliza muhula wake mwishoni mwa mwezi huu.

Wote wanatajwa kuwa na uzoefu wa hali juu katika masula ya kidiplomasia na wamefanya kazi kwa miaka mingi ndani ya mashirika ya Umoja wa Mataifa