Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi Mahiga awasihi wabunge wa Somalia kuendeleza upeo ulofikiwa sasa kisiasa Somalia

Balozi Mahiga awasihi wabunge wa Somalia kuendeleza upeo ulofikiwa sasa kisiasa Somalia

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustine Mahiga, amewasihi wabunge katika bunge jipya la Somalia kutumia fursa na wadhfa walio nao ili kuweka msingi bora kwa ajili ya siku za baadaye za taifa hilo la Pembe ya Afrika, wakati wa kumchagua rais mpya mnamo siku ya Jumatatu Septemba 10.

Kupitia barua wazi ambayo imechapishwa kwenye tovuti ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Balozi Mahiga amesema kuwa baada ya miongo ya vita, taifa kusambaratika na matukio mengi ya kudunisha utu na fahari ya watu wa Somalia, siku ya kumchagua rais itakuwa ni wakati muhumu kwao, kwani kitakuwa ndicho kikomo hasa kabisa cha kipindi cha mpito, na mwanzo wa kipindi cha mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa Somalia sasa imepiga hatua kubwa na kufikia kiwango cha juu kisiasa, na kwamba wabunge hao ni lazima wajitolee kudumisha kiwango hicho, kwa kufanya uchaguzi wa mtu anayefaa kama rais, na kuepukana na shinikizo za hongo ambazo zimedaiwa kuwa jinamizi kubwa katika siasa za Somalia. Katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa, Balozi Mahiga amemwambia Joshua Mmali ni nini kilichomfanya aandike barua hiyo