Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya kupinga na kuzuia kujiua kuadhimishwa tarehe 10 mwezi huu

Siku ya kimataifa ya kupinga na kuzuia kujiua kuadhimishwa tarehe 10 mwezi huu

Tarehe 10 mwezi Septemba ni siku kimataifa ya kuzuia kujiua ambapo hamasisho za kuzuia kujiua zitatolewa kote duniani. Makadirio yanaonyesha kuwa karibu watu 3000 hijiua kila siku kote duniani. WHO inasema kuwa inawasi wasi kutokana na kuongezeka kwa visa vya kujiua miongoni mwa vijana walio kati ya miaka 15 na 25. Kulingana na WHO vitendo vya kujiua sasa ndiyo vimeongoza kwa kusababisha vifo kwa watu wa rika hii. Hali ngumu za kiuchumi , kuvunjika kwa familia, unywaji wa pombe ni baadhi ya masuala ambayo huchochea watu kujiua huku nchi zilizo mashariki mwa Ulaya, India, china na Syria zikiandisha viwango vya juu vya watu wanaojiua. Tarik jasarevic kutoka WHO anaeleza

(SAUTI YA TARIK JASEREVIC)