Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yashangazwa na kusamehewa kwa mwanajeshi raia wa Azerbaijan

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yashangazwa na kusamehewa kwa mwanajeshi raia wa Azerbaijan

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea mshangao wake kutokana na kuachiliwa kwa mwanajeshi mmoja raia wa Azerbaijani ambaye alimpiga na kumuua afisa mmoja raia mmoja wa Armenia wakati wa mafunzo ya shirika la kujihami la nchi na magharibi NATO.

Ramil Safarov alisafirishwa kutoka Baku kwenda Hungary ambapo amekuwa akitumia kifungo cha maisha kufuatia mauaji hayo yaliyofanyika mwaka 2006. Ofisi ya haki za binadamu inasema kuwa kisa hicho kilichochewa na tofauti ya rangi. Alipowasili nyumbani Safarov alisamehewa na kupandishwa cheo hadi Meja baada ya kulakiwa kwa shangwe. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa hatua ya serikali ya Azerbaijan inatoa ishara mbaya ya uhusiniano kati ya mataifa hayo mawili. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)