Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2012

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2012

Je, wewe ni kijana ambaye amehitimu na shahada ya digrii, na unaongea lugha ya Kiingereza au Kifaransa sanifu? Je, ungependa kufanya kazi na Umoja wa Mataifa? Mtihani wa vijana waliobobea kitaaluma, na ambao wangependa kujiunga na Umoja wa Mataifa kwa mpango wa vijana waliobobea, yaani YPP, utafanyika Disemba 12, 2012.

Kuna nafasi katika idara kadha wa kadha za Umoja wa Mataifa, ikiwemo idara ya habari, ambako watayarishaji wa vipindi wanahitajika katika lugha za Kireno na Kiswahili.

Ili kushiriki mtihani huu, ni lazima uwe unatoka nchi zilizoorodheshwa kushiriki mwaka 2012, na ufanye ombi kushiriki kabla ya tarehe 12 Septemba. Paulina, ambaye ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, anaeleza zaidi kuhusu mtihani huu, na maandalizi yake.

(SAUTI YA PAULINA)

Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti:

https://careers.un.org