Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO lazungumzia hali ya wafanyikazi katika ukanda wa Gaza

ILO lazungumzia hali ya wafanyikazi katika ukanda wa Gaza

Shirika la kazi duniani ILO limezungumzia hali ya wafanyikazi kwenye eneo lililotwaliwa la wapaletina baada kijana mmoja wa kipaletina kujiteketeza moto baada ya kutafuta kazi kwa miezi kadha. Ihab Abu Nada kijana wa umri wa miaka 20 kutoka Gaza alikufa kutokana na majera mabaya aliyoyapata baada ya kujiteketeza hadharani Juma lililopita.

Kulingana na vyombo vya habari Abu Nada alikuwa amechoshwa na kutafuta kazi ndipo akaamua kujiteketeza kupinga hali iliyo kwenye ukanda wa Gaza. Kulingana na ILO hali kwa wafanyikazi kwenye ukanda wa Gaza ndiyo mbaya zaidi duniani. Kwenye ripoti iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu ILO ilionya kuwa ukosefu wa zjira miongoni mwa wapalestina na kukwama kwa mpango wa amani mashariki ya kati huenda vikasababisha madhara zaidi.