Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kipindupindu unazidi kusambaa zaidi magharibi mwa Afrika:UM

Ugonjwa wa kipindupindu unazidi kusambaa zaidi magharibi mwa Afrika:UM

Shirika la afya duniani WHO na lile la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF yameonya kuwa huenda hali ya sasa ya ugonjwa wa kipindupindu magharibi mwa Afrika ikawa mbaya hali ambayo huenda ikachochewa na mvua pamoja na mafuriko. Tayari mwaka huu jumla ya visa 55,289 vimeripotiwa kwenye nchi 15 na watu 1,109 kuaga dunia.

Ugonjwa huu unasambaa kwa haraka kwenye nchi zilizo katika bonde la mto Mano zikiwemo Guinea, Liberia na Sierra Leone na paia katika mto Congo na hivyo kuaathiri watu nchini Congo na kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na pia magharibi mwa Niger. Visa vilivyoripotiwa mwaka huu vya ugonjwa wa kipindupindu vimeongezeka kwa asilimia 34 ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka 2011 huku mvua zikitarajiwa kuchochea zaidi hali hiyo.