Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwawezesha, wanawake na wanaume pia ni muhimu kwa uzazi wa mpango:UNFPA

Kuwawezesha, wanawake na wanaume pia ni muhimu kwa uzazi wa mpango:UNFPA

Iwapo wanawake wakawezeshwa na kufikiwa kirahisi na huduma zinazosukuma kuwepo kwa uzazi wa mpango ni karata muhimu ambayo inakwamua hali ya kifedha na hivyo kuifanya jamii kuwa imara. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu duniani UNFPA.

UNFPA inasema kuwa katika mazingira ya kawaida suala la uzazi wa mpango linatizamwa kama ni jukumu la mama pekee lakini katika ukweli wa mambo lazima pande zote zihusike tena kwa kuwawezesha wanawake kunaweza kuleta tija zaidi.

Shirika hilo linaona kuwa kuwawezesha kina mama kufikiwa na huduma za afya hasa zile zinazoangazia uzazi wa mpango, ni hatua muhimu ambayo inaweza kufaulu kuwa na jamii inayozingatia matakwa ya uzazi wa mpango.