Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya chakula haijabadilika tangu Julai:FAO

Bei ya chakula haijabadilika tangu Julai:FAO

Thathimini ya bei ya chakula iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO inaonyesha hakuna mabadiliko toka mwezi wa Julai na pointi zimesalia kuwa 213.

Akiwasilisha tathimini hiyo ya bei kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Roma mkurugenzi mkuu wa FAO Jose’ Graziano da Silva amesema hali hii inatia matumaini ingawa bado watu wanatakiwa kuwa makini. Amesema bei za sasa hazidhihirishi kuondoka kwa matatizo ya chakula lakini jumuiya ya kimataifa inaweza kuingia kwenye soko lililotulia kiasi. Mtazamo wa bei ya chakula ulipanda kwa asilimia 6 Julai baada ya kushuka kwa miezi mitatu mfululizo.

(SAUTI YA GRAZIANO da SILVA)