Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR aonya juu ya hatari ya kutochukua hatua dhidi ya Mali

Mkuu wa UNHCR aonya juu ya hatari ya kutochukua hatua dhidi ya Mali

Kamishina Mkuu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR Antonio Guterres ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi za kupata suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Mali akionya kwamba kanda nzima itaathirika endapo hatua hazitochukuliwa.

Akizungumza katika taarifa iliyochapishwa na gazeti la New York Times Guterres amesisitiza kwamba hali ya Mali hivi sasa ni muhimu zaidi ya wakati mwingine wowote. Ameongeza kuwa taifa hilo la Afrika yawa kwani machafuko katika nchi hiyo ni tishio la utulivu wa kisiasa katika kanda nzima. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)