Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kutoweka kwa lazima kwa watu kuizuru Pakistan

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kutoweka kwa lazima kwa watu kuizuru Pakistan

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya kutoweka kwa lazima kwa watu linatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Pakistan kuanzia tarehe 10 hadi 20 mwezi Septemba kwa mwaliko wa serikali. Wakati ya ziara hiyo wataalamu hao watakusanya habari kuhusu madai kuhusu kutoweka kwa lazima yaliyo mikononi mwao.

Pia watachunguza hatua zilizochukuliwa na serikali katika kumaliza visa vya kutoweka kwa lazima. Kundi hilo litazuru sehemu tofauti za nchi na kukutana na maafisa wa serikali pamoja na waakilishi wa mashirika ya umma, familia za waliotoweka na waakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa. Kundi hilo baadaye litaanda mkutano baada ya kukamilisha ziara yake tarehe 20 Septemba mjini Islamabad kabla ya ripoti kuhusu ziara hiyo kuwasilishwa mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka ujao.