Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni ya IKEA na UNICEF yaadhimisha miaka 10 ya Ushirikiano

Kampuni ya IKEA na UNICEF yaadhimisha miaka 10 ya Ushirikiano

Ushirikiano wa zaidi ya miaka kumi kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF na kampuni moja ya Sweden iitwayo IKEA, katika kuwasaidia watoto nchini India unaadhimishwa mwezi huu, limesema shirika la UNICEF leo.

Kwa mujibu wa shirika hilo, sekta ya kibinafsi inatekeleza wajibu muhimu katika masuala ya kibinadamu na maendeleo. Limeongeza kuwa mashirika ya UMoja wa Mataifa yanaweza, na ni lazima yahusishe sekta ya kibinafsi, ambayo ilichangia dola milioni 155 kwa shughuli za UNICEF katika mwaka 2011.

Meneja Mkuu wa ushirikiano wa kimataifa katika UNICEF, John Winston amesema, kampuni za kibinafsi kama IKEA zimechangia pakubwa katika shughuli zake za kuwasaidia watoto kote duniani.