Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua kubwa zapigwa katika mazungumzo ya Bangkok kabla ya kongamano la Doha kuhusu hali ya hewa:UNFCCC

Hatua kubwa zapigwa katika mazungumzo ya Bangkok kabla ya kongamano la Doha kuhusu hali ya hewa:UNFCCC

Mazungumzo ya wiki moja kuhusu hali ya hewa yamekamilika leo mjini Bangkok, huku hatua muhimu zikipigwa na vikundi vyote vitatu vilivyohusika katika mazungumzo hayo. Ufanisi wa mazungumzo hayo unaweka msingi mathubuti kabla ya maazimio yatakayofikiwa kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ambalo litafanyika mjini Doha, Qatar mwaka huu.

Msimamizi Mkuu wa Mwongozo wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, Christiana Figueres, amesema kuwekeza katika mazungumzo ya Bangkok kumezaa matunda, na kwamba wawakilishi wa serikali mbalimbali katika mazungumzo hayo wamepigia debe masuala muhimu kwa njia ambayo wengi hawakutarajia, na kuongeza matumaini ya hatua ya ufanisi itakayofuata katika mkutano wa Doha.

Amesema bado kuna uamuzi mgumu wa kisiasa mbeleni, lakini sasa kuna msukumo wenye matumaini, na ari ya pamoja ambayo itachagiza mijadala katika viwango vya juu mjini Doha, na kuongeza kasi ya kutenda mambo. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)