Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto kubwa na kemiliki:UNEP

Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto kubwa na kemiliki:UNEP

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP hii leo limezindua ripoti kuhusu athari za kiaya na za kimazingira zinazosababishwa na kemikali zinazotengezwa na kutumiwa kote duniani. Kulingana na ripoti hiyo gharama ya athari za sumu inayotokana na madawa yanayotumiwa kwenye kilimo kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara ni ya juu kuliko misaada ya kimaendeleo inayotolewa kila mwaka kwa eneo hilo. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alihudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo na ametuandaliwa taarifa ifuatayo.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Ripoti hiyo inasema kuwa ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa gharama ya magonjwa kutokana na sumu za kemikali kwa wakulima wadogo kusini mwa jangwa la sahara kati ya mwaka 2005-2020 itakuwa dola bilioni 90. Uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo ni ya aina yake unajiri baada ahadi zilizotolewa na mataifa kwenye mkutano wa Rio+20 uliondaliwa mwezi Juni za usimamizi mwafaka wa taka zinazoathiri mazingira na afya ya binadamu. Mounkaila Goumandakoye ni mkurugenzi wa UNEP kanda ya Afrika na anasema kuwa bado bara la Afrika liko nyuma katika kukabiliana na athari za kemikali.

(SAUTI YA MOUNKAILA GOUMANDAKOYE)

“Kwa bahati mbaya lengo hili la kupunguza hatari hii ifikapo mwaka 2020 kwa bahati mbaya ulimwengu hasa bara la Afrika haliko kwenye lengo hili. Hatuko kwenye lengo hili kwa sababu utafiti kwa mfano kwa madawa ya kuua wadudu ni kwamba kurundikana kwa madawa ya kuuawa wadudu katika bara hili ni karibu tani milioni 50 na hadi sasa tunakabiliwa na changamoto kubwa jinsi ya kushughulikia kemikali hizo.”

Watu sehemu mbali mbali za dunia hasa kwenye mataifa yanayondelea wanategemea kwa ukubwa bidhaa zenye kemikali kwa mfano mbolea, bidhaa za elektroniki na hata plastiki kwa maendeleo yao ya kiuchumi. Lakini kulingana na Professor Geoffrey Wahungu ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika la mazingiza nchini Kenya NEMA ni kwamba Afrika imejipata matatani baada ya kushindwa kudhibiti baadhi ya kemikali ilizo nazo.

(SAUTI YA PROF. GEOFFREY WAHUNGU)