Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzuia ndio kitovu cha wajibu wa kulinda:Rais wa Baraza Kuu

Kuzuia ndio kitovu cha wajibu wa kulinda:Rais wa Baraza Kuu

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Ali-Nasser amesema Jumatano kwamba kupitia utekelezaji wa wajibu wa kulinda jukumu la Umoja wa Mataifa sio kuchukua nafasi ya serikali katika kutimiza wajibu wao wa kisheria wa kulinda.

Al-Nasser ameyasema hayo katika mjadala maalumu kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu wajibu wa kulinda maisha ya watu. Ameongeza kuwa wajibu wa kulinda unatumika kama muongozo wa kuzisaidia serikali ambazo haziwezi kutimiza majukumu yake ya kulinda watu wake.

Amesema jumuiya ya kimataifa itachukua hatua pale ambapo serikali au taifa linashindwa kulinda raia wake, hivyo hatua ya jumuiya ya kimataifa itakuwa ni katika kukumbusha na kusaidia na sio kuingilia uhuru wa nchi. Hii amesema ni lazima isaidie serikali ili kuhakikisha kwamba watu wao wanalindwa kikamilifu na kuzuia tafrani kabla haijatokea ndio kitovu kikubwa cha wajibu wa kulinda.