Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zatakiwa kuhakikisha usawa unapatikana kwa watu maskini

Serikali zatakiwa kuhakikisha usawa unapatikana kwa watu maskini

Umoja wa Mataifa unaona kuwa kuwepo kwa usawa juu ya haki ni kipengele mojawapo ambacho kinafungamana moja kwa moja na suala la haki za msingi za binadamu.

Hata hivyo Umoja huo wa Mataifa unataka usawa huo ufikiwe kwa watu maskini na makundi ya watu yaliyopo pembezoni.

Kulingana na mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya umaskini uliokithiri Magdalena Sepúlveda mataifa ya dunia yanapaswa kuchukua hatua mujarabu kuyawezesha makundi hayo yanafikiwa na usawa.

Amesema makundi ya watu maskini pamoja wale waliopembezoni nayo yana haki ya kufikiwa na masuala muhimu ikiwemo kupata fursa ya kuneemeka na usawa.