Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kuwa mbaya:ILO

Ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kuwa mbaya:ILO

Viwango va ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana vinasemekana vitakuwa vibaya zaidi duniani kote wakati matatizo ya kichumi na kifedha yakizidi kusambaa barani Ulaya kutoka kwenye mataifa yaliyoendelea kuelekea kwa nchi zinazochipukia kichumi.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kazi duniani ILO ilioyochapishwa Jumanne ambayo inamulika mtazamo wa kazi duniani na matarajio ya soko la ajira kwa vijana.

Mtazamo huo unaonyesha kwamba athari za matatizo ya kichumi barani katika ukanda wa Euro zinasambaa hadi Asia Mashariki na nchi za Amerika ya Kusini, zikifanya hali kwa mbaya zaidi wa wanaotafuta kazi.ILO inasema kimsingi ni katika mataifa yaliyoendelea tuu viwango vya tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana vinatarajiwa kupungua katika miaka ijayo.

Je kwa upande wa Afrika mambo yakoje? Theodoor Sparreboom ni mchumi katika shirika la ILO kitengo cha matarajio ya ukosefu wa ajira kwa vijana katika mataifa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

(SAUTI YA THEODOOR SPARREBOOM)