Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano kuhusu utokomezaji wa silaha za maangamizi linakabiliwa na utata mkubwa:Uswizi

Kongamano kuhusu utokomezaji wa silaha za maangamizi linakabiliwa na utata mkubwa:Uswizi

Taifa la Uswizi limesema kuwa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu uondoaji wa silaha linakabiliwa na utata mkubwa, na kwamba limeshindwa kuendelea mbele. Mjumbe wa Uswizi kwenye kongamano hilo amesema kuwa hali hiyo ni lazima iondolewe na kongamano hilo kutimiza jukumu lililokabidhiwa.

Taifa hilo limeishukuru Ujerumani kwa kutoa mswada wa mapendekezo, na kuelezea matumaini yake kwamba utakubaliwa na kupitishwa haraka. Limeongeza kuwa ilikuwa muhimu kwa ripoti hiyo kuonyesha kuwa kongamano limekuwa kwenye hali ya utata, na kwamba hakukuwa na hatua yoyote iliyokuwa imepigwa katika mwaka mmoja uliopita kujiondoa kwenye hali hiyo. Limesema mswada huo unaonyesha hali wastani baina ya kauli zilizopo katika mkutano na muafaka unaostahili kukubaliwa na wote.