Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Ebola wadhibitiwa Uganda huko DR Congo ukiendelea:WHO

Ugonjwa wa Ebola wadhibitiwa Uganda huko DR Congo ukiendelea:WHO

Ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa magharibi mwa Uganda unaelekea kudhibitiwa kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO. WHO inasema kuwa hakujaripotiwa visa vyovyote vya ugonjwa huo siku za hivi majuzi. Mkurupuko wa ugonjwa huo hatari uliripotiwa kwenye wilaya ya Kabaale magharibi mwishoni wa mwezi Julai ambapo umesababisha vifo vya watu 17 tangu wakati huo.

WHO inasema kuwa hakuna visa vyovyote vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa mwezi Agosti na kuongeza kuwa kumekuwa na ufuatiliaji wa kila siku kwa ugonjwa huo jinsi inavyohitajika. WHO inasema kuwa mkurupuko wa Ebola magharibi mwa Uganda hauna uhusiano wowote na mkurupuko wa ugonjwa huo ulioripotiwa kwenye mkoa wa Oriental mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao pia uliua jumla ya watu 11.

Wakati huohuo hadi kfikia tarehe 28 Agosti mwaka huu jumla ya visa 24 vya homa ya ebola vimebainika, sita vikitarajiwa, sita vimethibitishwa, 12 vikikisiwa na watu 11 wameripotiwa kufariki dunia kwenye jimbo la Orientale imesema WHO.