Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kuendesha utafiti wa kiafya kwa wahamiaji wa mataifa ya Kusini mwa Afrika

IOM kuendesha utafiti wa kiafya kwa wahamiaji wa mataifa ya Kusini mwa Afrika

Shirika la kimataifa la uhamiaji nchini Afrika Kuisni linatarajiwa kuendesha utafiti wa kiafya kwa watu wanaohama kutoka Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika wakielekea kanda ya Afrika Kusini. Utafiti huo ambao utang’oa nanga mwezi Septemba utaongozwa na shirika la kimataifa la utafiti la Lawry na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka ujao.

Utafiti huo utatoa mwelekeo wa sera kwa nchi zinazoathiriwa na uhamiaji ili ziweze kukabiliana vilivyo na changamoto zinazoletwa na uhamiaji. Utafiti huu unajiri kutokana na mapendekezo kwenye mkutano kuhusu usalama kwa wakimbizi na uhamaijai wa kimataifa uliondaliwa mjini Dar es Salaam nchini Tanzania mwaka 2010. . Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR  JUMBE)