Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakamilisha kuwasafirisha watu 2700 wanaorejea Sudan Kusini

IOM yakamilisha kuwasafirisha watu 2700 wanaorejea Sudan Kusini

Mashua nane za mwisho zinazowasafirisha zaidi ya watu 2700 na mizigo yao zinatarajiwa kutia nanga kwenye bandari ya Juba baada ya majuma matatu ya safari kutoka eneo la Renk kwenye jimbo la Upper Nile. Mashua hizo ziliondoka eneo la Renk ambapo bado raia 16,000 wa Sudan Kusini wamekwama mnamo tarehe kumi mwezi huu zikipitia kwenye bandari katika jimbo la Upper Nile na Jonglei zikielekea mji mkuu.

Wafanyikazi wa IOM waliwafanyia uchunguzi wale waliokuwa wakirejea nyumbani kubaini iwapo wako salama kusafiri na kuzuia magonjwa kuambukiza huku watoto walio chini ya miaka mitano wakichanjwa. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)