Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM una wasi wasi wa matumizi ya nguvu kupita kiasi nchini Guinea

UM una wasi wasi wa matumizi ya nguvu kupita kiasi nchini Guinea

Ofisi ya haki binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi mjini Conakry nchini Guinea.

Mapema juma hili kuliripotiwa makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani kwenye mji wa Conamry ambapo kulifyatuliwa risasi na watu kujeruhiwa. Makabiliano hayo yanajiri kufuatia mauaji ya watu 6 na wanajeshi tarehe tatu mwezi huu kwenye mji wa Zogota kusini mashariki mwa nchi . Serikali inaendesha uchunguzi kufuatia mauaji hayo ili kuweza kuwachukulia hatua wahusika.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)