Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF watoa ufadhili wa dola milioni 950 kufadhili oparesheni nchini Syria

CERF watoa ufadhili wa dola milioni 950 kufadhili oparesheni nchini Syria

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola milioni 950 kufadhili oparesheni za kibinadamu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Syria. Fedha hizo zinatarajiwa kuwasaidia wahamiaji 650 waliokwama wasio na njia nyingine ya kurudi nyumbani kuukimbia mzozo. Kati ya wahamiaji hao ni wanawake wafanyikazi wa nyumbani waliopelekwa Syria na mashirika ya kazi ambapo wengi wamepoteza ajira kutokana na mzozo wakiwa sasa hawana pesa na njia ya kurudi nyumbani.

Hadi sasa IOM imewasaidia wahamiaji wafanyikazi 1035 kutoka nchi 17 kurudi nyumbani . Chini Syria wahamiaji 83 wamekamilisha mipango yao na wanasubiri kuondoka Syria mara kutakapopatikana usafiri wa ndege. IOM inaendelea kupokea ombi kutoka kwa balozi mbali mbali kuwasaidia wahamiaji waliokwama nchini Syria.