Wakimbizi zaidi kutoka Syria waendelea kuwasili nchini Lebanon

31 Agosti 2012

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa kuna ongezeko kwa wakimbizi kutoka Syria wanaowasili mashariki bonde la Bekaa nchini Lebanon ikikadiriwa kuwa takriban watu 2,200 wamewasili eneo hilo juma lililopita. Hata hivyo wakimbizi wanaowasili kaskazini mwa Lebanon wamesalia kuwa ni watu 400 wanaowasili kila siku.

UNHCR inaweka laini mpya za simu ili kuwawezesha wakimbizi wanaoendelea kuongezeka wanaohitaji kujiandikisha. Msukosuko ulioshuhudiwa wiki iliyopita haukuwaruhusu wakimbizi kujiandikisha. UNHCR pia inachunguza hali ya wakimbizi katika eneo la Akkar ambalo hadi sasa linakumbwa na mashambuilizi kutoka Syria . Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud