Ban akaribisha kutolewa ripoti juu ya ubadilishanaji madaraka Maldives

31 Agosti 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anafurahishwa na kukaribisha ripoti iliyotolewa na kamishna ya Maldives iliyoundwa kuchunguza mazingira yaliyosababishwa kubadilishwa madaraka kulikofanyika mwezi February mwaka huu.

Kwa mujibu wa msemaji wake, Ban amezitolea mwito pande zote kukubali matokeo hayo ya ripoti hiyo na kuweka vinyongo pembeni na kuanza utekelezaji wake.

Ametaka pia pande zote katika duru la kisiasa kuanzisha majadiliano ya mezani ili hatimaye kustawisha demokrasia ya taifa hilo.

Mwezi February mwaka huu, raias wa wakati huo Mohamed Nasheed alilazimika kuachia madaraka kufuatia siku kadhaa za maandamano kutisho kutoka vikosoi vya kijeshi na askari polisi

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud