Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECHO yaipiga jeki IOM kutekeleza miradi ya wahamiaji Zimbabwe

ECHO yaipiga jeki IOM kutekeleza miradi ya wahamiaji Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji nchini Zimbabwe IOM limepokea kiasi cha euro milioni 1 kutoka kwa kamishna ya Umoja wa Ulaya inayozingatia masuala ya dhaura na usamaria mwema ECHO.

Kiwango hicho cha fedha kinatazamia kusaidia kukamilisha mradi ambao umelenga kuwafadhilia jamii ya wahamiaji ambao wapo kwenye mkwamo.

Sehemu kubwa ya mradi huo imewalenga jamii ya Wazimbabwe walioko upande wa kusin mashariki mwa nchi hiyo ambao watapatiwa motisha kuwafadhilia wale waliokosa makazi. Zimbabwe inatajwa kuwa kitovu cha wakimbizi wa aina mbalimbali wale wanatumia eneo hilo kusafiri kwenda nchi nyingine na wale wanaosalia nchini humo wakiwa hawana ustawi bora wa maisha.