Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia nchini Syria wanakabiliwa “maangamizi ya kimkakati”

Raia nchini Syria wanakabiliwa “maangamizi ya kimkakati”

Kundi ya raia nchini Syria ikiwemo watoto na wanawake wanakabiliwa na kile kinachoelezwa na afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa “ maangamizi ya kimkakati”

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson kiasi cha watu milioni 2.5 ikiwemo wakimbizi wa Kipalestina na Iraq wapo kwenye maisha ya taabu na dhiki kubwa.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la usalama kilichowajumuisha pia mawaziri wa mambo ya nje na maafisa wa Umoja wa Mataifa , Naibu Katibu huyo ameeleza kundi hilo la watu ndani ya Syria linahitaji msaada wa dharura.

Ameonya uwezekano wa kujiri hali mbaya zaidi iwapo kutakosekana kwa utashi wa kusitisha mapigano hayo.